Skip to main content

Familia ya Rubani wa DP Ruto Yadai Haki

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

This archive report was first published on 14 July 2019.

Wakati wa mazishi ya rubani wa DP Ruto, Marius Magonga, familia yake ilizungumza kuhusu ajali ya ndege iliyomuua kufanya hima. Mazishi hayo yalifanyika Mabonde katika Kaunti ya Trans Nzoia Jumamosi, Julai 13.

Abdulmalik Magonga, ndugu wa rubani huyo, alisema familia hiyo ingali inasumbuliwa na ajali hiyo kwani hawajawahi kupata matokeo rasmi ya kilichofanyika na kusababisha ndege hiyo kuanguka.

Abdulmalik alisema ndugu yake alikuwa rubani mwenye tajriba na hawajaelewa ni vipi alikubali kupaa angani nyakati za usiku kinyume.

"Hatujui kilichosababisha ndege hiyo kuanguka, na kile tunaomba ni uchunguzi wa kina kufanywa na shirika la huduma za ndege nchini (KCAA). Tunahitaji matokeo kamili ili tukumbali yaliyotokea," Abdulmalik alisema.

Rubani Magonga alifariki mnamo Machi 3, 2019 wakati ndege yake ilianguka katika eneo la Lobolo Kaunti ya Turkana alipokuwa amewapeleka watalii katika kisiwa kimoja eneo jilo.

Polisi walitoa taarifa kwamba ndege hiyo ilikuwa na watu watano na wote waliangamia baada ya kuanguka mwendo wa saa mbili usiku.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →