Uchaguzi mkuu ujao ni fursa ya kubadilisha mienendo ya siasa nchini yetu. Tunapaswa kutumia busara na kufanya maamuzi sahihi ili kuchagua viongozi wastaarabu.
Ustaarabu ni kipengele muhimu cha demokrasia, na tunapaswa kuhakikisha kuwa viongozi wetu wana ustaarabu na heshima kwa wote.
Wanasiasa wanaotumia kila mbinu kuhakikisha wamechaguliwa, lakini baadhi yao wakitoa kauli zinazokosa ustaarabu, heshima na demokrasia katika siasa zetu.
Uhuru na demokrasia ya kisiasa tunaojivunia nchini yetu inafaa kulindwa kwa kuhakikisha tunazingatia maadili ya umoja, upendo na amani katika taifa letu.
Wananchi wanafaa kuchukua hatua katika uchaguzi mkuu ujao waamue kuwakataa viongozi wachochezi, wakabila, wanafiki na waliofeli kutekeleza ahadi zao kikamilifu.
Maadamu Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) haina mamlaka ya kuwazuia viongozi hao kuwania nyadhifa mbalimbali, ni raia tu wanaweza kuwazima viongozi wakorofi katika siasa zetu kwa kuwachagua viongozi wangwana na waadilifu.