Skip to main content

Alex Olaba, Mchezaji wa Raga ya Kenya, Asakwa kwa Madai ya Ubakaji

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

This archive report was first published on 13 July 2019.

Alhamisi, jaji Martha Mutuku alitoa ilani ya kukamatwa kwa Alex Olaba, mchezaji wa zamani wa timu ya Kenya Harlequins, kwa kukosa kufika kwenye kesi ya ubakaji inayomkabili na mwenzake Frank Wanyama.

Uamuzi wa kesi hiyo ulikuwa umepangiwa Alhamisi, lakini Olaba alikosa kufika na kulazimisha kikao cha kesi kuahirishwa hadi Ijumaa.

Wanyama alifika kwenye kesi, lakini Olaba alikosa kufika na jaji Martha Mutuku alitoa ilani ya kukamatwa kwake.

Olaba na Wanyama walishakiwa kwa kosa la kumbaka Wendy Kemunto mnamo Februari 2018, katika mtaa wa Highrise Kaunti ya Nairobi.

Wachezaji hao wa timu ya Kenya Harlequins hawajakuwa wakicheza tangu kesi hiyo kuwasilishwa kwenye kesi na hii ni baada ya Muungano wa Raga nchini kuamrisha wasijumuishwe katika kikosi cha timu hiyo kucheza hadi kesi dhidi yao isikizwe na kuamliwa.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →