This archive report was first published on 12 July 2019.
Usiku wa Jumatano, Julai 10, 2019, afisa wa polisi Abdinasir Harun alikuwa hotelini kula chakula cha jioni baada ya kutoka eneo la ajali iliyokuwa imetokea kabla.
Wanaume watano waliojihami kwa silaha waliingia ghafla na kuamrisha kila mtu kulala chini. Harun alipigwa na kifaa butu kabla ya wavamizi hao kutoroka na bunduki yake.
Kamanda wa trafiki wa Machakos alivamiwa na kunyang'anywa bunduki wakati akila chakula cha jioni hotelini.
Abdinasir Harun alivamiwa na wanaume watano katika soko la Katheka Kai. Majambazi hao wakafanikiwa kuchukua bastola yake aina ya Cesca.
Harun alikimbizwa Hospitali ya Machakos Level Five kabla ya kuhamishiwa Hospitali ya Nairobi South anakoendelea kutibiwa.
Polisi wameanzisha msako kuwanasa waliotekeleza uvamizi huo na kutoroka na bastola ya mwenzao.