This archive report was first published on 11 July 2019.
Alhamisi Julai 11, 2019, Mbunge wa Nyakach Aduma Owuor alikamatwa na maafisa wa upelelezi wa Tume ya Maadili na Kupambana na ufisadi (EACC) akiwa mjini Kisumu.
Alipokamatwa, Aduma alikuwa akihojiwa na makachero wa EACC kwa saa kadhaa kuhusiana na madai ya ufisadi kuhusu malipo yasiyo ya kawaida ya KSh 68 milioni kwa kampuni moja ya sheria katika kaunti ya Nairobi.
Alitakiwa kuhamishwa hadi Nairobi kufanyiwa uchunguzi zaidi.
Aduma aliyafanya malipo hayo wakati alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa mambo ya kisheria katika kaunti ya Nairobi.