This archive report was first published on 11 July 2019.
Naibu Rais William Ruto atashinda urais iwapo atanyenyekea mbele ya Wakenya, amesema Mbunge wa Tiaty William Kamket.
Amesema Ruto amekuwa na kiburi sana jambo ambalo ni kinyume kwa mtu yeyote anayetafuta nafasi ya kuwa rais wa Kenya.
Alisema hili siku ya Jumatano, Julai 10, wakati akiwa na wafuasi wa chama chake KANU.
“Nguvu za kisiasa hazitachukuliwa kwa nguvu, kuwa mnyenyekevu mbele ya Wakenya. Wacha hizi sarakasi za eti mtu anataka kukuua. Kuna mtu anazunguka Kenya kana kwamba ameumwa na nyoka mbaya, tafadhali nyenyekea na uzungumze na Wakenya. Uongozi ni kunyenyekea,” alisema mbunge huyo.
Wakati huo huo, Kamket alitangaza kuwa seneta wa Baringo Gideon Moi anajitayarisha kuwania urais katika uchaguzi wa 2022.