Skip to main content

Maaskofu wa ACK Mumias Wapiga Marufuku Mazishi ya Wikendi

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

This archive report was first published on 11 July 2019.

Maaskofu wa Kanisa la Kiangilikana la diosisi ya Mumias wamepiga marufuku mazishi ya wikendi, kwa ajili ya kuwazuia wanasiasa kuingilia kati na kutatiza shughuli za mazishi.

Imeonekana kuwa hafla nyingi za mazishi zinapigwa wikendi, na wanasiasa wanapata fursa ya kupiga siasa badala ya kuacha familia zilizofiwa kuomboleza mpendwa wao.

Askofu wa kanisa hilo Joseph Wandera alisema uamuzi huo umefanywa baada ya mashauriano na watahakikisha kwamba hafla yoyote ya mazishi inafanywa siku za wiki pekee.

"Tunawatambua na tunawajali wanasiasa wetu ila ibada za mazishi zimekuwa zikiingiliwa sana na wanasiasa na kufanya zikose umuhimu, tutazidi kuwatambua wanasiasa wetu lakini hatutakubali watatize hafla zetu za mazishi," Wandera alinukuliwa na Nation.

Maaskofu hao wataendesha hafla za mazishi siku za Jumatatu hadi Ijumaa pekee.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →