This archive report was first published on 9 July 2019.
Wabunge Wanashinikiza Marupurupu ya Nyumba ya KSh. 250,000 ¶
Wabunge wa Kenya wanaashinikiza kulipwa marupurupu ya nyumba ya KSh. 250,000, huku wengine wakidai kuwa mishahara yao ni duni zaidi.
Seneta wa Kiambu Kimani Wamatangi alisema kwamba anapokea mshahara wa KSh 640 kila mwezi, huku akidai kuwa anategemea biashara zake kwa mahitaji ya familia yake pamoja na gharama zingine.
Wabunge wengine ambao wamelalamikia mishahara duni ni pamoja na mbunge wa Rarieda Otiende Amollo na mwenzake wa Homa Bay Peter Kaluma.
Wabunge hawa wamejitokeza na kuelezea kwa nini mishahara yao ni duni, huku wakishinikiza kulipwa marupurupu ya nyumba ya KSh. 250,000.
Seneta Wamatangi alisema kwamba anachukua mikopo ambayo hukatwa kwenye mishahara yake, huku akidai kuwa angekuwa ananyanyaswa na makali ya njaa kama hangekuwa na mbinu za kibiashara ambazo zimemwezesha kukimu maisha yake.
Alidai kuwa changamoto wabunge wanazo pitia zinachangiwa na taarifa za kupotosha zinazotolewa kwa umma kuwa wabunge wana pesa nyingi kwa hivyo hawahitaji marupurupu.
Wabunge wengine pia wamejitokeza na kuelezea kwa nini mishahara yao ni duni, huku wakishinikiza kulipwa marupurupu ya nyumba ya KSh. 250,000.