Skip to main content

Wakenya Waorodheshwa Katika Nafasi ya Pili Kwa Urembo Barani Afrika

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

This archive report was first published on 9 July 2019.

Wakenya wameorodheshwa katika nafasi ya pili barani Afrika kwa urembo, kulingana na utafiti uliofanywa na shirika la Big 7. Nchi ya Afrika Kusini ilishikilia nafasi ya kwanza.

Utafiti huo ulitumia kigezo cha Lupita Nyong'o, mshindi wa tuzo la Oscar, kama kigezo cha kuwaorodhesha Wakenya katika nafasi hiyo.

Kenya iliorodheshwa katika nafasi ya kumi na nne, huku Afrika Kusini ikiishikilia nafasi ya sita kote ulimwenguni.

Ukrain ilishikilia nafasi ya kwanza katika ripoti hiyo ya Big 7, kwa sababu ya urembo na mvuto wa kipekee wa wananchi wa nchi hiyo.

Wananchi kutoka Denmark, Ufilipino, Brazil, na Australi walishikilia nafasi za pili, tatu, nne, na tano mtawalia.

Timu hiyo iliwashirikisha watu 1.5 milioni ambao walitakiwa kutoa mtazamo wao na kupiga kura kuhusiana na mdahalo huo.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →