Skip to main content

Mbinu za Kudhibiti Vifaabebe: Mbinu za Kudhibiti Watoto Kwenye Mitandao ya Kijamii

N

Nyakundi Report

Newsroom 2 min read

This archive report was first published on 16 January 2022.

Matumizi ya mitandao ya kijamii yanaongezeka na madhara yake kwa watoto yanaendelea kubainika. Hata hivyo, watalaamu wa malezi dijitali wanasema kuna mbinu zinazoweza kutumiwa na wazazi kudhibiti taarifa ambazo watoto wao wanatazama na muda wanaoweza kutumia mtandao.

Programu za kusaidia kudhibiti kizazi kipya cha digitali zimeundwa na wanasema zinasaidia wazazi kuwadhibiti watoto wao mtandaoni kwa urahisi zaidi. Mbinu hizi zinaweza kuunganishwa kwa WiFi na kudhibitiwa mtu akiwa mbali na nyumbani kuhakikisha watoto wanalindwa na madhara ya kutazama habari na picha hatari kwenye mitandao ya kijamii.

“Kuna programu za kusaidia kudhibiti kizazi kipya cha digitali na waliounda wanasema zinasaidia wazazi kuwadhibiti watoto wao mtandaoni kwa urahisi zaidi,” asema mtaalamu wa masuala ya malezi dijitali, Sarah Kingston. “Kuna mifumo kama mduara wa Disney, Koala Safe na Ikydz, ambayo inadaiwa kuwa na uwezo wa kudhibiti kila kifaa cha dijitali katika nyumba kupitia programu ya ‘smartphone’.

Programu hizi zinaweza kuunganishwa kwa WiFi na kudhibitiwa mtu akiwa mbali na nyumbani kuhakikisha watoto wanalindwa na madhara ya kutazama habari na picha hatari kwenye mitandao ya kijamii. Mzazi pia anaweza kuchuja matumizi ya vifaa vya kidijitaji kulingana umri wa watoto.

“Kwa mfano, unaweza kuzuia watoto wako kutafuta wapenzi mtandaoni na kucheza kamari kwa kudhibiti vifaa vya kidijitali nyumbani hata ukiwa mbali kwa kuwa kuna programu zinazokuwezesha kuona wanachofanya na kila kifaa kupitia simu yako,” aeleza Kingston.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →