Skip to main content

Uhaba wa Mahindi Ukiendelea, Bei ya Ungwa Kupanda

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

This archive report was first published on 5 January 2022.

Bei ya unga kupanda kwa haraka, na wasagaji mahindi wanaona bei ya mahindi kupanda kwa Sh3,000 kwa gunia moja la kilo 90.

Wakati wa msimu wa uvunaji mahindi, bei ya unga imekuwa Sh100 kwa pakiti ya kilo mbili, na wasagaji mahindi wanaona bei ya mahindi kupanda kwa Sh3,000 kwa gunia moja la kilo 90.

Wakulima wengi hawataki kuyauza mahindi yao wakati huu kwani bei za zao hilo bado ziko chini.

“Kwa wakulima wengi, huo ni mkakati wa kibiashara. Wanataka kuyauza mazao yao wakati bei zitakapopanda ili kupata faida,” alisema Tim Njagi, mtafiti wa kilimo katika Taasisi ya Utafiti na Sera ya Tegemeo.

Wizara ya Kilimo imepewa barua na Muungano wa Wasagaji Mahindi Kenya (UGMA) kuhusu ongezeko la bei ya unga na bei ya mahindi kupanda.

UGMA inasema kuwa kwa sasa, wasagaji wananunua gunia moja la mahindi kwa Sh3,000 ikilinganishwa na Sh2,800 hapo awali.

Wizara ya Kilimo inasema kuwa uzalishaji mahindi utapungua kwa asilimia 20 msimu huu, kutokana na mvua chache na athari za viwavijeshi walioyashambulia mashamba mengi ya zao hilo mwezi Machi.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →