This archive report was first published on 2 January 2022.
Ujauzito ni mchakato changamano ambao unaweza kuwa na matatizo mbalimbali. Kuvuja damu wakati wa ujauzito katu si dalili nzuri, na hii ni kwa sababu mzunguko wa kihomoni kila mwezi umekatizwa.
Ukuta wa uterasi ambao huambuka kila mwezi wakati wa hedhi sasa unatumika kumkuza mtoto aliye tumboni. Hata hivyo, unaweza kuvuja damu wakati wa ujauzito, wakati ambapo mimba inajitundika kwenye ukuta wa uterasi.
Damu hii hutoka wiki za awali za ujauzito na kwa kawaida haitoki kwa wingi. Aidha, unaweza kuvuja damu kutokana na mwasho kwenye lango la uzazi, au ikiwa kuna maambukizi, au ikiwa mimba imejitundika nje ya uterasi (ectopic pregnancy), au ikiwa kuna hatari ya mimba kutoka.
Matatizo haya huhitaji kuangaliwa na mwanajinakolojia. Aidha, huenda uchunguzi wa maabara ukahitajika na wakati mwingine kupigwa picha ya sehemu ya nyonga.
Ujauzito ni mchakato changamano ambao unaweza kuwa na matatizo mbalimbali. Kuvuja damu wakati wa ujauzito katu si dalili nzuri, na hii ni kwa sababu mzunguko wa kihomoni kila mwezi umekatizwa.