Skip to main content

Uunganishaji haramu wa stima waweka wakazi gizani miezi 12

N

Nyakundi Report

Newsroom 2 min read

This archive report was first published on 1 January 2022.

MAKALA MAALUM: Uunganishaji haramu wa stima waweka wakazi gizani miezi 12

Wakazi wa mitaa kadhaa ya mashariki mwa kaunti ya Nairobi, hasa ya mabanda eneo la Mukuru, wanaishi gizani baada ya kampuni ya Kenya Power kuondoa transfoma eneo hilo kwa kuhangaishwa na matapeli.

Msako uliofanywa na wafanyakazi wa kampuni hiyo ya kusambaza stima, wakishirikana na maafisa wa polisi waliojihami kwa bunduki, ulikuwa na lengo la kuwaweka watu wanaounganishia stima kiholela na kinyume cha sheria.

Msako uliendeshwa kuanzia mtaa wa mabanda wa Mukuru-Kwa Njenga, Mukuru-Kwa Reuben, Mukuru-Sinai, Mukuru-Paradise, Mukuru-Jamaica, Mukuru-Lunga Lunga, na Mukuru-Doonholm, na kisha hadi mtaa wa Mukuru-Kingstone na Mukuru-Tetra Pak.

Matapeli walikuwa wakiunganishia stima wakazi na kuwatoza ada ya kati ya Sh500 na Sh1,000 kulingana na mahitaji.

“Ikiwa utawekewa stima kwa nyumba, walitoza Sh500 kwa kila mwezi. Ikiwa stima yako itawekwa saluni au duka iliyo na jokovu, ulilazimika kuwalipa Sh1,000 kwa mwezi,” alisema mkazi mmoja wa mtaa wa Mukuru Kayaba.

Hasara ya kampuni ya Kenya Power ilionekana kufuatia hatua ya matapeli kuunganisha stima kinyume cha sheria na kuhatarisha wakazi na mali yao.

“Wanaoiba stima ni matajiri wakubwa ikizingatiwa kuwa hakuna ushuru hutozwa kwao wala hakuna peni inaingia kwa serikali. Kampuni huripoti hasara ya mamilioni ya pesa kufuatia kuharibika kwa transfoma zilizolipuka baada ya kubebeshwa moto kupita kiasi,’’kampuni inasema kwenye ripoti.

Transfoma zaidi ya 20 ziliondolewa mitaani na kubebwa wakati wa msako huo.

Matumaini yameanza kuonekana katika mtaa wa Mukuru-Kwa Reuben, ambapo stima imerudishwa kupitia mradi wa serikali wa kuunganisha wakazi stima wa Last Mile.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →