Skip to main content

Wanariadha waalikwa kushiriki Mbio za Nyika za Mombasa

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

This archive report was first published on 30 December 2021.

Chama cha Riadha cha Kenya (AK) tawi la Mombasa linaalika wanariadha kutoka shule, vyuo na mashirika mbalimbali kushiriki kwenye Mbio za Nyika za Mombasa zinazofanyika Januari 8.

Wanariadha hawa watakuwa wakimbiaji wa timu ya Mombasa watakayochaguliwa kwenye mbio hizo ili kuwakilisha kaunti hiyo kwenye Mbio za Nyika za Pwani zinazotarajiwa kufanyika Januari 15.

“Tunataka kuwasilisha timu ya wakimbiaji mahiri kwani tunataka wengi wao wachaguliwe kwenye kikosi cha timu ya Pwani kitakachoshiriki kwenye Mbio za Nyika za Kitaifa zinazotarajiwa kufanyika Januari 22,” anasema Anisa Abdalla, mwenyekiti wa tawi hilo la AK Mombasa.

Timu za kaunti mbalimbali za Pwani zikiwemo za Kwale, Kilifi, Lamu, Tana River, Taita Taveta na Mombasa zinajitayarisha kuhakikisha wanariadha wao wanachaguliwa kwenye kikosi cha timu ya eneo hilo kushiriki michezo ya kitaifa.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →