This archive report was first published on 23 December 2021.
Na Richard Munguti
Mahakama kuu iliposimamisha kesi ya Bilionea Humphrey Kariuki na washukiwa wengine saba kwa kukwepa kulipa ushuru wa Sh17 bilioni, jaji Antony Mrima alimwagiza hakimu mkuu Kagendo Michemi akome kusikiza kesi hiyo.
Jaji Mrima alisema Bw Kariuki amehoji uhalali wa kesi inayomkabili akisema mamlaka ya ushuru nchini haipasi kuruhusiwa kuongoza kesi hiyo, ilhali ndiyo iliichunguza.
Kesi hiyo ilikuwa inalenga kesi ya kukwepa kulipa ushuru wa Sh17 bilioni, ambayo Bw Kariuki alisema haki zake zimekandamizwa kwa vile sheria za ushuru nchini zaipa KRA uwezo wa kuamua masuala yote kuhusu ushuru.
Jaji Mrima atasikiza kesi hiyo Februari 10, 2022.