This archive report was first published on 21 December 2021.
Mwanamke Abakwa na Kutupwa Kwa Maji Machafu Mukuru ¶
Usiku wa Jumapili, Jumapili, Desemba 19, 2021, mwathiriwa alikuwa akipika na kuuza samaki mtaani jirani wa Kaiyaba kabla ya kuhamia mtaani wa Maasai.
Bi Jane Mbula Kyalo, mhudumu wa masuala kuhusu dhuluma za watoto na wanawake mtaani, aliongeza kwamba mwathiriwa alipatikana na wamama wanaouza mboga mtaani mwendo wa saa tisa za asubuhi huku nao wasiwajulishe watu.
Wahudumu wa afya waliowasili kwa ambulensi walimchukua mwathiriwa na kumpeleka hospitalini kwa matibabu.
Ndani ya nyumba ya mwathiriwa, majirani walisema huishi peke yake tangu ahamie mtaani huo.
Bi Jane aliongeza kwamba alijulishwa kuhusu tukio hili mwendo wa saa tano za mchana na ndipo akasimamisha shughuli zake za nyumbani ili amshughulikie mwathiriwa.