Skip to main content

Wanabodaboda Thika wahimizwa kuweka akiba kwa vikundi

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

This archive report was first published on 18 December 2021.

Wanabodaboda wameshauriwa kujisajili rasmi ili waweze kutambulika na kuweza kupata mikopo kupitia J-Hela.

Mbunge wa Thika, Patrick 'Jungle' Wainaina, amewahimiza wanabodaboda kujiunga kwa vikundi ili kuweza kutambulika na kuweza kupata mikopo kupitia J-Hela.

Alipongeza pendekezo la Inspekta Jenerali wa Polisi, Hilary Mutyambai, kwamba wanabodaboda wanafaa kujisajili rasmi ili wajulikane popote walipo.

Wanabodaboda wameshauriwa kujisajili rasmi ili waweze kutambulika na kuweza kupata mikopo kupitia J-Hela.

Idadi ya wanachama katika vikundi hivyo ni 4,000 katika eneo la Thika.

Alieleza kuwa iwapo kila mmoja ataweka kwenye akiba Sh100 akiwa katika kikundi bila shaka hata mwaka mmoja watapata zaidi ya Sh1 milioni.

“Mimi ningetaka kuona mhudumu wa bodaboda anatoka katika kiwango hicho na kujinunulia gari lake. Pia ningetaka kuona kila mmoja akijitegemea kibinafsi,” alifafanua mbunge huyo.

Wanabodaboda wameshauriwa kujisajili rasmi ili waweze kutambulika na kuweza kupata mikopo kupitia J-Hela.

Alipongeza jinsi walivyohamasishwa kuhusu kuweka akiba ili kujiendeleza kimaisha.

“Sisi kama wanabodaboda tumekuwa hatuna maarifa ya kuweka akiba lakini wakati huu tumepata mwongozo utakaotupatia mwelekeo bora. Tukitoka hapa ni lazima tujipange kwa vikundi ili tuanze kuweka akiba polepole,” alisema Bw Mwangi.

Wanabodaboda wameshauriwa kujisajili rasmi ili waweze kutambulika na kuweza kupata mikopo kupitia J-Hela.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →