This archive report was first published on 6 July 2019.
Julai 5, 2019: Mbunge wa Molo Kimani Kuria amewaomba wakaazi wa eneo hilo msamaha baada ya kuwasili kwenye mkutano wa kujadili utumizi wa pombe akiwa mlevi chakari.
Waakazi waliachwa vinywa wazi na wakaanza kumzomea mbunge huyo baada ya kubaini alikuwa mlevi kutokana na mienendo yake wakati akiwahutubia.
Aliomba msamaha kwa kuhudhuria hafla akiwa mlevi katika ujumbe aliouchapisha kwenye ukurasa wake wa Facebook.
Aliasisitiza kuwa alihitaji kusikiliza wenzake na kushirikiana na wafuasi wake ili kushughulikia masuala ya eneo lake.
Aliahidi kurejelea miradi ya maendeleo katika eneo bunge lake na kuhakikisha kwamba wenyeji wa Molo wananufaika.
Aliomba msamaha kwa kuhudhuria hafla akiwa mlevi na kuhakikisha kwamba hatua hiyo itachukuliwa kwa kujitolea.