Skip to main content

Wazazi, Walezi Wazungumze na Watoto Wao Likizo Hii Fupi

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

This archive report was first published on 19 November 2021.

Shule zinafungwa leo kwa likizo fupi, na yatarajiwa kuwa wanafunzi watakaa na wazazi na walezi wao na kubadilishana mawazo yanayohusu maisha yao shuleni.

Waketi na wana wao na kuwadadisi kuhusu matatizo yanayowakumba na kuwapa ushauri nasaha pamoja na kuwakidhia mahitaji yao ili kuepusha ghasia na visa vya kuteketeza mali ya shule.

Wanafunzi wanaotekeleza uovu huu ni watoto wetu, na tunahitaji kujibu maswali kuhusu kwa nini wanafunzi hawa watundu wanahusika katika uhuni na uhalifu huu bila kuogopa.

Je, wanafunzi hawa watundu wanajua uchungu wa jamii katika kugharimia ukarabati wa madarasa ambayo walichoma?

Tangazo la waziri wa Elimu Profesa George Magoha kuwatwika mzigo mzito wazazi kugharimia ukarabati na ujenzi wa majengo yanayoteketezwa na wanafunzi lasikitisha na kuatua moyo.

Si hatua ya busara na tangazo hilo halitaisaidia lolote bali litazidisha malumbano baina ya serikali, wazazi na hata walimu.

Wazazi hapaswi kubebeshwa zigo la dhambi za mwanawe shuleni.

Tunahitaji kuwa na njia mbadala ya kushughulikia zahama hii.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →