This archive report was first published on 18 November 2021.
‘Sekta za kilimo, ufugaji ziimarishwe vijana wapate kazi’ ¶
Wazazi wanaoendeleza kilimo-biashara katika shamba lenye ukubwa wa ekari 30, wana wazazi wapata kazi kupitia duka lao, Forujo Fresh Veggies, ambalo linalingana na Nairobi Farmers Market (NFM) katika kusaidia wakulima kufikia wateja.
Wazazi hao ni wakulima hodari wa nyanya, pilipili mboga za rangi tofauti, vitunguu, matango na celery-kiungo kinachofanana na dhania.
Wanadada hao, Joyce Gichana na Ruth Wakonyo, wana umri wa miaka 24, wamekuwa wakisaidia wazazi wao kutafutia soko mazao wanayozalisha eneo la Ruai, Kaunti ya Nairobi.
“Tumekuwa katika kitengo cha mauzo,” Joyce adokeza.
Wanadada hao wanasoma, Joyce ana Shahada ya Digrii katika Masuala ya Uhusiano mwema wa Umma (Public Relations) na Saikolokia, naye Ruth amesomea Digrii ya Uhusiano wa Kimataifa na kuipiga jeki kwa Uhusiano mwema wa Umma.
“Tulituma maombi chungu nzima kuomba kazi katika kampuni na mashirika tofauti, ila hatujawahi kupata mwaliko wa ajira,” Ruth asema.
Jeff Mundia, meneja wa soko hilo, pia ni mmoja wa wanaomiliki duka, The Farm Outlet, ambalo hulima matunda aina ya mapapai, karakara, ndizi, avokado na matikitimaji.
“Ili kukwepa kero ya mazao kuharibika na kuoza, huyaongeza thamani kwa kuunda sharubati ya matunda na viungo vinginevyo,” Jeff afichua.
Fairtrade Africa (FTA), shirika linalounganisha wakulima na kampuni wanachama wake kwa soko la mazao katika nchi za kigeni, linasema bidhaa zilizoongezwa thamani zina ushindani mkubwa.
“Mazao yaliyoungezwa thamani, mapato yanakuwa hadi mara tatu,”anasema Kate Nkatha, Mkurugenzi Mkuu wa Mauzo FTA, akihimiza wakulima kukumbatia mfumo wa uongezaji thamani.