Skip to main content

Daktari asema hakupata sumu katika mwili wa Tecra

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

This archive report was first published on 12 November 2021.

Mei 2, 2020, ilikuwa siku ya kifo cha Tecra Patricia Muigai, mrithi wa kampuni ya kutengeneza pombe ya Keroche Industries. Kesi inayochunguza kifo chake inajadiliwa mahakamani.

Bw James Matinde, mtaalamu wa maabara ya serikali, alipima sampuli sita kutoka kwa mwili wa Tecra, alisema hakupata sumu yoyote ambayo ingechangia katika kifo chake.

Alisema pia hakupata kileo chochote katika sampuli iliyotolewa kwenye jicho la Tecra. "Sikupata hata chembe za pombe katika Vitreous Humor (sampuli kutoka kwa jicho la Tecra)," alisema alipohojiwa na wakili maarufu wa Mombasa, Bw Yusuf Abubakar.

Usiku ambao Tecra alianguka, mpenziwe Omar Lali aliambia polisi kwamba, walikuwa wametafuna miraa na kubugia pombe aina ya Smirnoff. Chupa mbili kubwa za pombe na ya Soda ya Fanta ziliwasilishwa kortini kama ushahidi.

Shahidi huyo aliongeza kuwa pombe inaweza kupatikana katika chembechembe za mwili saa nane tu baada ya mtu kuaga dunia. Bw Matinde alisema jinsi mwili unavyozidi kukaa ndivyo pombe inazidi kuyeyuka kwenye damu na sehemu zingine mwilini.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →