Skip to main content

OCS wa Muthaiga Simamishwa Kazi baada ya Picha za Dennis Itumbi Kupigwa Kituoni

N

Nyakundi Report

Newsroom 2 min read

This archive report was first published on 5 July 2019.

Simamisho la Kazi la OCS wa Muthaiga

Alphonce Kemengua, OCS wa Muthaiga, amesimamishwa kazi kwa muda baada ya picha za Dennis Itumbi kupigwa kituoni na rafiki zake wakiwa stesheni.

Itumbi, ambaye ni katibu wa mawasiliano ya maswala ya ughaibuni katika afisi ya Rais, alikamatwa mnamo Jumatano, Julai 3, kwa tuhuma za kuandika barua feki iliyodai kuwepo njama ya kumwangamiza Ruto na kuisambaza mitandaoni.

Alipofikishwa katika mahakama ya Milimani, Alhamisi Julai 4, alidokeza kuwa alikuwa na video ikionyesha baadhi ya viongozi katika Hoteli ya La mada kunakodaiwa njama ya kumuua Ruto ilijadiliwa.

Itumbi alisema, "Mkurugenzi wa uchunguzi wa makosa ya jinai DCI ana haja na ukweli. Wanataka nikiri kwamba niliandika hiyo barua. Naweza kuicheza hiyo video mahakamani kuthibitisha kwamba mkutano ulifanyika, lakini hawana haja na ukweli," alisema Itumbi.

Wakati uo huo, alimwomba hakimu Zainab Abdul, kuwaamuru Polisi wamzuilie katika kituo cha Polisi cha Muthaiga au cha Kileleshwa, akidai kuwa wachunguzi wa kesi yake walitaka kumzuilia katika kituo cha Polisi cha Kamkunji na wahalifu sugu.

Alphonce Kemengua alipokea barua yake ya kusimamishwa kazi kwa muda Ijumaa, Julai 5, kutokana na kile ambacho ilisemekana kuruhusu picha kupigwa kituoni.

Itumbi alikamatwa na makachero kwa tuhuma za kuandika barua feki iliyodai kuwepo njama ya kumwangamiza Ruto na kuisambaza mitandaoni.

Alipofikishwa katika mahakama ya Milimani, Alhamisi Julai 4, alidokeza kuwa alikuwa na video ikionyesha baadhi ya viongozi katika Hoteli ya La mada kunakodaiwa njama ya kumuua Ruto ilijadiliwa.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →