Skip to main content

Wahalifu Mtandaoni Kuchukuliwa Hatua

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

This archive report was first published on 5 November 2021.

Uzinduzi wa Kamati ya Kitaifa ya Kupambana na uhalifu mtandaoni ulifanyika jana Alhamisi, November 4, 2021, katika Taasisi ya Kuboresha Mitaala ya Elimu ya KICD jijini Nairobi.

Waziri wa Masuala ya Ndani, Fred Matiang'i, alisema kwamba serikali itawakamata wahalifu mtandaoni bila huruma, na kuweka kipaumbele ulinzi wa taarifa za kibinafsi za kampuni, watoto, na nchi kwa jumla.

Alisema, "Kwa miaka mingi, watu wamekuwa wakikandamizwa mtandaoni. Maneno ya uongo na ya kuchochea chuki yanasambazwa mtandaoni. Wahalifu wengi hawajapata kuchukuliwa hatua. Lakini baada ya uzinduzi huu, tutawakamata bila huruma."

Kamati hiyo inajumuisha wasimamizi kutoka wizara ya masuala ya ndani, Mawasiliano, wapelelezi wa makosa ya jinai, vitengo mbalimbali vya maafisa wa polisi na mahakama kuu.

Waziri Matiang'i alitaka kamati hiyo itoe mafunzo kwa Tume ya Huduma za Mahakama kuhusiana na masuala ya mtandao na jinsi ya kuwaadhibu wahalifu hao.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →