Skip to main content

Wiki ya Ubunifu nchini kuanza Desemba 6

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

This archive report was first published on 5 November 2021.

Wiki ya Ubunifu nchini kuanza Desemba 6

Wiki ya Ubunifu nchini itafanyika kuanzia Desemba 6 hadi Desemba 10, 2021 eneo la Lower Kabete, Nairobi. Wiki hii itakuwa na lengo la kuonyesha ubunifu wa Wakenya na kuendeleza miradi ya nchi chini ya Ajenda Nne Kuu na Ruwaza ya 2030.

Wiki ya Ubunifu itajumuisha mikutano minne ya; ubunifu unaoegemea ujuzi na talanta, teknolojia na mabadiliko kwa viwanda, biashara na uanzilishaji.

Waziri wa Elimu, Profesa George Magoha alisema kuwa wiki ya ubunifu itasaidia kugeuza mwelekeo wa elimu na utafiti pamoja na kuimarisha maendeleo katika taasisi na kustawisha jamii na uchumi.

“Wiki hii ya ubunifu itawafaa wabunifu na wanaweza wavutia watega-uchumi, washiriki au hata wateja. Tunawaomba wote walio na bidhaa na huduma walizobuni waje wazionyeshe,” alisema Mwenyekiti wa Shirika la Ubunifu nchini (KeNIA), Dkt Tonny Omwansa.

Wiki ya Ubunifu itawapa motisha Wakenya na kuwawezesha kuwa na ujuzi wa ubunifu, kwa kusema wa Bi Sheena Raikundalia, Mkurugenzi wa Kitovu cha Teknolojia cha Uingereza nchini Kenya.

Wiki ya Ubunifu itawaleta pamoja wakuu kutoka serikali za kaunti, sekta binafsi, washiriki wa maendeleo, wanaounda sera, wanahabari na jamii kwa jumla ili kuwafaa Wakenya.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →