Skip to main content

Familia ya Profesa Hassan Nandwa inamtaka Rais Kenyatta kuamuru kuachiliwa kwa msomi wa kiislamu

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

This archive report was first published on 31 October 2021.

Wasiwasi wa familia ya Profesa Hassan Nandwa

Profesa Hassan Nandwa, msomi wa kiislamu aliyedaiwa kutekwa nyara na maafisa wa polisi Alhamisi, sasa ana wasiwasi mkubwa kwa familia yake.

Wakiongea na wanahabari Jumamosi, Oktoba 30, 2021, mkewe msomi huyo Bi Mawahib na mwanawe wa kiume Elmiqdad Hassan wamejawa na wasiwasi mkuu tangu kutoweka kwa msomi huyo Alhamisi jioni.

"Tunamheshimu sana Rais wetu Uhuru Kenyatta kama kiongozi ambaye anaheshimu Katiba na sheria za nchi zinazolinda haki za rai wote. Ndio maana tunamwomba aamuru maafisa wa polisi kumwachilia huru Profesa Nandwa ili ashtakiwe rasmi ikiwa alitenda kosa lolote. Sio haki kwa maafisa wa usalama kuendelea kumzuilia," Bi Mawahib akasema huku akibubujikwa machozi.

Awali Jumamosi, viongozi wa kiislamu wameitaka serikali kukomesha visa vya utekwa nyara wa waumini wa dini hiyo kwa tuhuma za ugaidi.

Profesa Nandwa ambaye pia ni wakili mtajika alidaiwa kutekwa nyara na watu waliodaiwa kuwa maafisa wa polisi kutoka kitengo cha kupambana na ugaidi mwendo wa saa kumi na mbili za jioni.

Alhamisi jioni, Profesa Nandwa alikamatwa baada ya kuhudhuria swala ya jioni katika msikiti wa Jamia, Nairobi. Hii ni baada ya kuhudumia wateja wake na kupiga ripoti katika kituo cha Central kuhusu kukamatwa tena kwa mteja wake mwingine aliyekamilisha kifungo chake majuzi.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →