Skip to main content

Hatutaunga Mwaniaji Urais Nje ya OKA, Vinara Wanasema

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

This archive report was first published on 30 October 2021.

Wakati wa mkutano wa vyama vya OKA mjini Kakamega, waliwakilisha vyama vyao Musalia Mudavadi (ANC), Kalonzo Musyoka (Wiper), Gideon Moi (Kanu), na Moses Wetangula (Ford Kenya).

Wakizungumza, walifichua kwamba kuna watu wenye ushawishi wanaowapigia simu wakitaka waunge mgombea wa urais nje ya OKA.

"Tupatie kila kiongozi nafasi ya kuuza manifesto yake ili Wakenya waamue kiongozi aliye na mikakati bora," alisema Musalia Mudavadi.

Alisema pia, "Hatutaruhusu yeyote atulazimishie uongozi. Hatutaruhusu yeyote kuwalazimishia Wakenya anayepaswa kuwa rais 2022."

Alipuuza mifumo ya uchumi inayotumiwa na Naibu Rais William Ruto na kiongozi wa ODM Raila Odinga kujipigia debe, Kalonzo Musyoka alisema kinachohitajika ni kupunguza ushuru unaotozwa Wakenya kwa asilimia 50.

"Tukipunguza ushuru kwa asilimia 50, uchumi utakuwa sawa na Wakenya watakuwa na pesa na kuacha kutegemea pesa chache wanazodanganywa nazo. Ajenda ya OKA ni kufufua uchumi na kuukuza pamoja na kujenga umoja na utangamano miongoni mwa Wakenya," alisema.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →