This archive report was first published on 4 July 2019.
Kijana aliyejaribu kuingia Ikulu akiwa amejihami kwa kisu aachiliwa kwa dhamana ya KSh 100k ¶
Alhamisi Julai 4, Hakimu Francis Andayi alimuamuru babake kwa masharti kuhakikisha Brian anapata matibabu ya kina ya kiakili katika hospitali ya rufaa ya Moi baada ya kesi yake kurejelewa Agosti 7.
Wakati Brian Bera alipofikishwa mbele ya mahakama, alikataa mashtaka dhidi yake, na kwa hivyo hakujibu mashtaka yoyote dhidi yake.
Alipofikishwa kizimbani kwa mara ya kwanza Jumatano Julai 3, mwanafunzi huyo wa mwaka wa tatu katika kitivo cha handisi alimwomba radhi Rais Uhuru Kenyatta kwa kosa alilofanya.
"Nina shida na nimeumia sana kukaa kwenye seli, ningependa Rais Uhuru Kenyatta na Wakenya kwa ujumla wanisamehe, sitarudia kosa hilo tena," Brian aliomba mahakama.
Wakati babake Bera, David Bera, alikariri kuwa, kutotumia dawa alizopewa na daktari kulichangia mwanawe kutaka kuingia Ikulu.
"Kumzuilia kwenye seli itamchukua muda kupona na pia hali yake kutobadilika,"alisema babake.
Source: Tuko News, 2019-07-04T19:22:31.000Z