Skip to main content

Matapeli Mtaani Wakatizwa Mradi wa Maji, Wakasababisha Uhaba wa Maji Shuleni na Mtaani

N

Nyakundi Report

Newsroom 2 min read

This archive report was first published on 27 September 2021.

Mradi wa maji unaotegemewa na wakazi wa mtaa wa Kayaba, Nairobi, umekatizwa na matapeli mtaani, kusababisha uhaba wa maji shuleni na mtaani.

Wakazi wa mtaa huo wamekosa maji kwa zaidi ya mwezi mmoja baada ya matapeli kudaiwa kuathiri mradi wa maji.

Mradi huo wa maji ni wa tatu kuwekwa katika maeneo ya South B, ikiwemo kisima cha St Bakhita na kile cha Hazina.

Wakazi katika mitaa ya Hazina na Kayaba huchota maji kutoka kwa visima hivyo bila malipo yoyote.

Matapeli wanaouza maji mtaani wa mabanda wa Kayaba wamejiunganishia maji na kusabisha hitilafu katika mashine ya kupiga maji.

“Baada ya mtambo wa maji kuvurugwa na wakiritimba mtaani waliojiunganishia maji kuelekea mtaani, mashine ya kupiga maji imeharibika,” alisema Bi Regina Nzomo, mkuu wa shule ya Msingi ya Sancta-Maria Mukuru.

Mradi wa maji ni wa tatu kuwekwa katika maeneo ya South B, ikiwemo kisima cha St Bakhita na kile cha Hazina.

Wakazi katika mitaa ya Hazina na Kayaba huchota maji kutoka kwa visima hivyo bila malipo yoyote.

Usimamizi wa shule umeiomba serikali kutuma waandisi ili kukarabati mashine ndiposa shule na wakazi wapate maji.

“Serikali ilichimba visima hivyo miongoni mwa vingine mitaani ya mabanda katika kaunti ya Nairobi ikilenga kuwapunguza wakiritimba ambao huwafyonza wananchi hela nyingi wanazotoza wakazi kutokana na huduma ya maji, stima na kodi ya nyumba,” alisema Bw Michael Aswani Were, mkuu wa tarafa ya South B.

Wakazi walikosa maji ya mgao kutoka siku ya Alhamisi hadi tukienda mitaboni.

Wachuuzi huuza maji kwa Sh5 kwa kila mtungi wa lita 20 lakini wakati kuna uhaba wa bidhaa hiyo, hupandisha na kuuza Sh10 na Sh20 kwa kila mtungi mmoja wa maji wa lita 20.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →