This archive report was first published on 25 September 2021.
Timu ya Vihiga Queens ilipokea Sh1 milioni kutoka kwa Gavana wa Kaunti ya Vihiga, Wilber Ottichilo, mnamo Septemba 25, 2021, kama ahadi yake baada ya kufuzu kuwa mwakilishi wa Cecafa kwenye makala ya kwanza ya Klabu Bingwa Afrika nchini Misri mwisho wa mwaka 2021.
Timu hiyo ilipata tiketi ya kushiriki kombe hilo baada ya kupepeta wanabenki wa CBE kutoka Ethiopia 2-1 kwenye fainali ya kusisimua ya Cecafa ugani Kasarani mnamo Septemba 9.
Shikangwa aliibuka mchezaji bora wa mashindano hayo yaliyovutia klabu nane kutoka mataifa ya Kenya, Ethiopia, Uganda, Tanzania, Burundi na Djibouti pamoja na Zanzibar.
Timu hiyo ya Kenya itawania taji la Klabu Bingwa Afrika dhidi ya wenyeji Wadi Degla SC (Misri), AS FAR kutoka Morocco (washindi wa Muungano wa Kaskazini mwa Afrika), AS Mande kutoka Mali (washindi shindano la kwanza la Muungano wa Magharibi mwa Afrika), Hasaacas Ladies kutoka Ghana (washindi shindano la pili la Muungano wa Magharibi mwa Afrika) na Rivers Angels (nambari mbili katika shindano la pili la Muungano wa Magharibi mwa Afrika).