This archive report was first published on 10 September 2021.
Polisi wamekamatwa washukiwa kumi wanaokabiliwa na mashitaka ya kufyonza mafuta katika bohari moja katika Eneo la Viwanda, Kaunti ya Nairobi mnamo Alhamisi, September 9, 2021.
Washukiwa hao walikuwa wakijaza mafuta aina ya dizeli, mafuta ya taa, na petroli katika bohari moja mkabala wa barabara ya Rangwe.
Maafisa wa polisi walionasa magari sita, jenereta tano, mitungi 97, pipa nne za diseli, mapipa saba ya mafuta taa, na pipa sita zikijaa mafuta ya taa na pipa moja likiwa limejaa nusu yake.
Maafisa wa polisi waliona mitungi 17 ya lita 20 kila moja bila kuwa na chochote ndani.
“Washukiwa wote kumi walipatikana wakijaza mafuta aina ya dizeli, mafuta ya taa na petroli katika bohari moja mkabala wa barabara ya Rangwe. Tumenasa magari yaliyohusika sawia na vifaa walivyokuwa navyo vya kufyonza mafuta,” alisema Bw. Timon Odingo, mkuu wa polisi katika divisheni ya Makadara.
Washukiwa hao wamefungwa katika kituo cha polisi cha Industrial Area huku uchunguzi zaidi ukifanywa.
“Tunachunguza kesi hii ili kuona ikiwa tutawakamatwa wote wanaohusika katika biashara hii haramu. Tunaamini hii biashara haramu imeendeshwa chini ya maji tangu miaka 20 iliyopita,” alisema Bw. Odingo.
Maafisa wa polisi waliona washukiwa wanaosha mifuko ya plastiki iliyotumika kutoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA) kisha wanaibadilisha kuunda bidhaa.
Magari yaliyonaswa ni pamoja na lori aina ya Mitsubishi Fuso KBC 167, Isuzu KAJ 805 L, Isuzu aina ya FRR-KBM 877B, pick-up KXT 492, lori la NMS-GK B 350W aina ya FAW, na lori aina ya Mitsubishi Fuso KCM 240 A.