This archive report was first published on 3 July 2019.
Julai 3, 2019 - Mwanamume mmoja amewasilisha mswada bungeni wa kutaka neno 'Harambee' kufutwa kwenye nembo ya Kenya kwa kudai kuwa ni ishara ya bahati mbaya kwa taifa.
Charles Koinange Mangua anadai kuwa alipata ufunuo kutoka kwa Mwenyezi Mungu kuwa, jina hilo litaleta majanga nchini endapo haitabadilishwa na jina 'Kenya'.
Alisema katika barua yake iliyosomwa na Spika wa Bunge la Kitaifa Justin Muturi, 'Nyinyi ndiyo mtabeba lawama binafsi mbele za Mwenyezi Mungu kuhusu jina hilo kwenye taswira ya urathi, ambayo ingepaswa kuandikwa Kenya.'
Aliongeza kuwa, 'Ombi langu kwa bunge la taifa ni kuwa watakuwa na kikao cha dharura ili kupitisha mswada huu ili sheria iweze kubadilishwa kuhusu jina hilo.'
Julai 3, 2019, neno 'Harambee' lilianzishwa na mashujaa waliopigania uhuru wa nchi hii kama ishara ya umoja.
Walakini, kwa miaka na mikaka kumekuwa na mapendekezo ya kutaka neno hilo kufutiliwa mbali kwani hakuna anayefahamu msingi wake.
Neno hilo linatumika sana nchini kama kielelezo cha alama ya nchi ikiwemo timu ya taifa ya Kenya, Harambee Stars.
Ofisi kuu za serikali ziko katika mtaa wa Harambee jijini Nairobi.
Wakati wa kuitengeneza katiba ya mwaka 2010, baadhi ya Wakenya walizua hoja hiyo ya kutaka jina hilo kundolewa.