This archive report was first published on 2 July 2019.
Wanawake wawili wa Liani, Machakos, walishuhudia sisema ya bure baada ya kulishana makonde hadharani wakizozania leso.
Wanawake hao walikuwa wamehudhuria sherehe iliyoandaliwa katika eneo hilo ambayo ilikuwa ya kufana mno.
Mapambano yalienda kombo pale ambapo kikundi cha akina mama kilianza kutunukiwa zawadi za leso, na wanawake hao walianza kubishania leso moja iliyokuwa imebaki.
Uvuta nikuvute hiyo ilishuhudiwa baina ya wanake hao ambapo kila mmoja alionekana kuvuta kamba upande wake akitaka awe ndio wa kutunukiwa.
Mzozo huo ulizidi na mama mmoja akamrukia na kumzaba kofi mwenzake huku akimfokea.
"Hii leso ni yangu. Mimi ndio nimefika hapa wa kwanza. Usiniletee nyenyenye zako," mama mmoja alisikika akimwambia mwenzake.
Source: Tuko.co.ke