Skip to main content

Corona Imenisukuma Kwa Kona: Dickson Muceri Amejikita Kwenye Mashambani

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

This archive report was first published on 9 July 2021.

Corona Imenisukuma Kwa Kona

Na SAMMY WAWERU

Corona imesababisha kushuka kwa sekta ya huduma za tuktuk, na Dickson Muceri, mmiliki wa tuktuk Githurai, amejikita kwenye mashambani.

Aliathiriwa kwa kiasi kikubwa na corona mwaka uliopita, na alikuwa mmiliki wa tuktuk mtaani Githurai, kiungani mwa jiji la Nairobi.

Aliingilia kitambo ili kujiendeleza kimaisha, lakini baada ya Machi 2020, sheria na mikakati kuzuia maenezi ya Covid-19, ugonjwa ambao sasa ni janga la kimataifa, sekta mbalimbali ziliathirika.

‘Baadhi ya wawekezaji katika sekta ya tuktuk walianza kuuza magari yao. Ni gari la jumla ya abiria watano ila Covid iliwashusha hadi wawili,’ asema Muceri.

Aliamua kupeleka familia yake mashambani, Kaunti ya Meru, ili kuokoa ndoa yake changa.

‘Niliuza tuktuk na kuanza mradi wa kujenga nyumba ili mke na mwanangu wawe salama,’ Muceri afichua.

Alijaaliwa mtoto wa pili na lazima ajikaze kiume kukithi familia yake riziki na mahitaji mengine muhimu ya kimsingi.

Maisha ya jiji la Nairobi, hasa baada ya nyongeza ya mafuta ya petroli, kodi ya bidhaa tofauti za kula, mitungi ya gesi, miongoni mwa nyingine, yamekuwa mchongoma kukwea.

‘Ninaendelea kufanya vibarua vinavyopatikana, vikiwemo vya huduma za mikahawa,’ asema Muceri.

‘Himizo langu kwa wanaopitia hali kama yangu wasilaze damu, wafanye vibarua vilivyopo muradi tu viwe halali,’ Muceri ashauri.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →