This archive report was first published on 1 July 2019.
Magazeti ya Jumatatu, Julai 1 ¶
Magazeti ya Jumatatu, Julai 1, yanaripoti kuhusu Naibu wa Rais William Ruto na kinara wa upinzani Raila Odinga wakirushiana cheche za maneno kuhusu kutoa michango kanisani.
Magazeti haya pia yanaripoti kuhusu mchakato unaoendeshwa na FBI kuhusu barua tata iliyokuwa inadai kuwa na njama ya kumdhuru Ruto.
Idara ya upelelzi nchini Marekani (FBI) ilimaliza kuifanya uchunguzi barua tatanishi iliyokuwa imesambazwa mitandaoni kuhusiana na madai ya kuwa na njama ya kumuangamiza Naibu wa Rais William Ruto.
Tayari idara hiyo iliwasilisha matokeo yake kwa DCI na sasa imeibuka kuwa lawama imewaondokea wandani wa Ruto na kuilenga idara yake ya mawasiliano.
Mkurugenzi mkuu wa idara ya mawasiliano katika ofisi ya rais (PSCU), Dennis Itumbi, ni miongoni mwa wale wanaosemakana kuhojiwa katika afisi ya DCI.
Itumbi yamekanusha madai hayo ya kuhojiwa kwa kudai kuwa yeye anafanya kazi chini ya rais bali sio naibu wake.
Wakenya wengi wanamlaumu Rais Uhuru Kenyatta ¶
Wakenya wengi wanamlaumu Rais Uhuru Kenyatta kuwa chanzo cha changamoto zote zinazokumba taifa hili.
Asilimia 26 ya Wakenya wanamlaumu Uhuru kwa ukosefu wa ajira na gharama ya juu ya maisha huku asilimia 15 wakiwakashifu wanasiasa wote.
Magazeti ya Kenya Jumatatu, Julai 1: Serikalo ya Uhuru, Ruto yaelekeza nchi pabay. Picha: UGC
Mwanamke kutoka Kangemi alitapeliwa na jamaa yake ¶
Mwanamke mmoja kutoka mtaa wa Kangemi jijini Nairobi alitapeliwa na jamaa yake baada ya kujifanya kuwa Gavana wa Nairobi Mike Sonko.
Alikutana na mwanamume huyo kwenye mtandao wa Facebook na alikuwa akidai kuwa alikuwa akiwatuza wakazi pikipiki ili kuwasaidia kujikimu maishani.
Alimuagiza mama huyo wa watoto wanne kumtumia KSh 2,000 ya kujisajili.
Alibadilisha njia ya mawasiliano kwa kuanza kumtongoza mama huyo na kumwambia mama huyo amtumie picha zake akiwa uchi jambo ambalo aliitikia kwa sababu ya tamaa.
Mama huyo alikuja kugundua baadaye kuwa alitapeliwa baada ya kuona ujumbe wa Sonko akiwaonya Wakenya dhidi ya matepeli ambao wanatumia jina lake kuwadanganya watu.
Wanafunzi wa chuo kikuu cha Stanford walikuwa wamekula chakula cha jioni ¶
Wanafunzi wa chuo kikuu cha Stanford, Norah Borus, alikuwa ameuwa chuoni humo.
Alizikwa mnamo Jumamosi, Juni 29.
Alisifiwa kama msichana mcha Mungu ambaye alipenda kuimba na kizicheza nyimbo za injili.
Viongozi ambao walihudhuria mazishi hayo walizuiliwa kutoeneza siasa katika hafla hiyo baada ya babake marehemu kudokeza kuwa mwanawe alikuwa anapenda masuala ya sayansi.
HELb inapokea pesa chache ¶
Bodi ya kutoa mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu HELB, inapania kupokea pesa chache kinyume na vile ilivyopendekeza katika mwaka wa kifedha wa mwaka 2019/20.
Itapokea KSh 12.6 bilioni kutoka kwa wizara ya fedha ili kusaidia idadi kubwa ya wanafunzi wa vyuo vikuu wanoitaji pesa hizo.
440,000 walionufaika na mkopo huu wamekaidi kulia na kuchangia katika deni kuongezeka hadi KSh 52.1 bilioni.
150,000 wanaendelea kulipa deni yao ambayo ni takriban KSh 23.6 bilioni.