This archive report was first published on 2 July 2021.
Timu ya taifa ya ndondi imeimarisha maandalizi yake kwa michezo ya Olimpiki, huku ikisalia na wiki mbili kuondoka nchini kueleka Tokyo, Japan.
Maandalizi haya yameimarishwa kwa kujumuisha wakufunzi wawili wenye tajriba katika mchezo huu, kama vile Ibrahim ‘Surf’ Bilali, mshindi wa nishani ya shaba katika Michezo ya Olimpiki ya mwaka wa 1984, na Charles Mukula, kocha wa klabu ya Dallas ya Muthurwa.
‘Hit Squad’ inayojumuisha mabondia Christina Ongare (fly), Nick ‘Commander ‘ Okoth (unyoya), Elizabeth Akinyi (welter) na Elly Ajowi kinatarajiwa kuondoka nchini Julai kuelekea Tokyo, Japan.
‘Tumekuwa tukirekebisha kasi na nguvu ya mabondia wetu katika mazoezi yetu na kumekuwa na mabadiliko makubwa,’ akasema kocha Musa Benjamin.
Na kwa mujibu wa kocha David Munuhe, kikosi ha ‘ Hit Squad ‘ inayojumuisha mabondia wanne waliofuzu kushiriki michezo ya Olimpiki wako katika hali nzuri na tayari kupeperusha bendera ya taifa jijini Tokyo, Japan.
‘Hakuna medali katika Olimpiki iliyowekewa bondia yeyote wala iliyo na jina kwa hivyo tunaenda nchini Japan kung’ang’ania medali hizo bila kuogopa kwa sababu tumejiandaa barabara,’ akasema nahodha Nick ‘Commander ‘ Okoth.
Michezo ya Olympiki inatarajiwa kung’oa nanga Julai 23 hadi Agosti 9, 2021.