Skip to main content

Wavuvi Lamu Wadai Maegesho Yao Yamenyakuliwa

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

This archive report was first published on 15 June 2021.

Wavuvi Lamu wanaona hatari kubwa kwa sekta yao ya uvuvi kwa sababu ya maegesho yao ya maegesho yanayodaiwa kunyakuliwa na mabwenyenye.

Maegesho hayo ya ekari moja ya wavuvi ni ya umma na imekuwa ikitumika kama maegesho ya wavuvi tangu ukoloni.

Ukuta tayari umejengwa kwenye maegesho hayo, hivyo kuwazuia wavuvi kuitumia.

“Tulipozaliwa tulipata wazee wetu tayari wakitumia maegesho haya. Tunavyojua ni kwamba ardhi ni ya umma na ilitengewa wavuvi tangu ukoloni. Tumeshangazwa na hatua ya mabwenyenye watatu ambao wamejitokeza kudai umiliki wa kipande hicho cha ardhii,” alisema Mwenyekiti wa Makundi ya Wavuvi (BMU) kisiwani Lamu, Abubakar Twalib.

Naibu Gavana wa Lamu, Abdulhakim Aboud, alisema mikakati inaendelea kwenye ofisi yake ili kuona kwamba maegesho ya wavuvi kote Lamu yanalindwa kupitia utoaji wa hatimiliki.

“Wavuvi wasiwe na shaka. Tunatarajia shughuli ya kutoa hatimiliki kwa maegesho ya wavuvi kote Lamu ianze wakati wowote,” alisema Bw Aboud.

Maafisa wa Tume ya Kitaifa ya Ardhi (NLC) wamejumuishwa katika mikakati hii ya kutoa hatimiliki.

Maegesho ya wavuvi kote Lamu yanadaiwa kuholewa na mabwenyenye, na hii inaweza kusababisha kukosa kupanuka kwa sekta ya uvuvi na samaki kote Lamu.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →