This archive report was first published on 15 June 2021.
Wavuvi wa Lamu wanasema maegesho yao ya wavuvi yameonyakuliwa na mabwenyenye, na kuwazuia kutumia ardhi hiyo ya umma.
Maegesho hayo ya wavuvi ya ekari moja, ambayo ndiyo maegesho ya pekee ya wavuvi iliyosalia mjini Lamu, inapatikana karibu na eneo la KenGen.
Wavuvi wanasema kuwa ardhi hiyo ni ya umma na imekuwa ikitumika kama maegesho ya wavuvi tangu ukoloni.
Ukuta tayari umejengwa kwenye maegesho hayo, hivyo kuwazuia wavuvi kuitumia.
Naibu Gavana wa Lamu, Abdulhakim Aboud, alisema kuwa mikakati inaendelea kwenye ofisi yake ili kuona kwamba maegesho ya wavuvi kote Lamu yanalindwa kupitia utoaji wa hatimiliki.
“Wavuvi wasiwe na shaka. Tunatarajia shughuli ya kutoa hatimiliki kwa maegesho ya wavuvi kote Lamu ianze wakati wowote,” akasema Bw Aboud.