This archive report was first published on 18 May 2021.
Na SAMMY WAWERU
Eneo la Gatumbiro, Ol Joro Orok, Kaunti ya Nyandarua, ni mahali ambapo Dison Wanjohi, mkulima mwenye ujuzi wa miaka 14, amejikita katika ukuaji wa miwa.
Ukulima wa miwa ni shughuli yenye matukio ainati, na Dison amejituma kukata kiu cha miwa kwa wenyeji eneo hilo.
Alipofanya utafiti wa kina, alionyesha kuwa Nyandarua ina hali bora ya anga na udongo kukuza miwa.
Alipata ujuzi huo mwaka wa 2005, na kuanzia kwa robo ekari, alianza kufanya jaribio.
Alitumia Sh10,000 pekee kuanza safari, na mwaka mmoja na miezi sita baadaye, mahesabu yake yaliingiana.
Utafiti aliozamia, na kuutekeleza kwa njia ya matendo, ukabainisha Nyandarua si tofauti na Mumias, Meru na Kisii.
Alipanda miwa yake kwa kutumia mbolea ya mifugo, na kwa sasa ana jumla ya ekari moja.
Alisema gharama yake ni nafuu na ya chini mno ikilinganishwa na ukuzaji wa mimea inayochukua muda mfupi kuzalisha.
Alisema miwa ni rahisi kupanda, na upanzi wa miwa unahitaji mashimo yenye urefu wa futi mbili kuenda chini na upana wa kipenyo cha futi mbili pia.
Alisema kilimo chake ni hai, kisichotumia fatalaiza wala dawa zenye kemikali.
Alisema changamoto za miwa ni haba mno, na kwa sababu ya barafu, miwa hukauka msimu wa baridi kali.