Skip to main content

Wanaharakati walaani hatua ya polisi kuwakamata waandamanaji Mombasa

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

This archive report was first published on 25 August 2020.

Maandamano ya wanaharakati waandamana kwa haki za binadamu katika Mombasa yalipaswa kuwa na matokeo mabaya baada ya maafisa wa polisi kuwakamata saba Jumanne asubuhi.

Waandamanaji hao walikuwa wakifanya maandamano wakitaka waporaji wa fedha za kupambana na janga la corona wakamatwe.

Maafisa wa polisi wamewatawanya wakidai kuwa walivunja sheria ya kutotangamana iliyowekwa na Wizara ya Afya kuzuia maambukizi ya virusi vya corona.

Wakizungumza nje ya kituo cha polisi, viongozi wa mashirika mbalimbali ya kutetea haki wamedai kuwa maafisa hao wa polisi wamekiuka sheria kwa kuwakamata wanaharakati hao waliokuwa wakifanya maandamano kwa amani.

“Wanawakamata watu wadogo na wanyonge kama sisi badala ya kuwakamata na kuwafunga viongozi wafisadi katika serikali,” amesema Padre Gabriel Dolan, mkurugenzi wa shirika la Haki Yetu.

Amesema Wakenya hawawezi kusahau maovu yanayoendelea “hata wakijaribu kutunyamazisha, tutazungumza kwa kuwa wakiiba fedha hizo, wanamwangamiza Mkenya ambaye anazihitaji.”

Maandamano kama hayo pia yalifanyika katika kaunti za Kisumu, Nakuru na Nairobi.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →