This archive report was first published on 21 August 2020.
Ukosefu wa kazi na uwezekano wa kupata riziki umeweka wajane na watoto wa Nyamira kwenye ulingo wa kupasua mawe.
Wanawake kutoka eneo la Gekomu, wadi ya Kemera, wamekuwa wakiifanya kazi hii kwa muda mrefu, lakini kwa watoto, kufungwa kwa shule na ukosefu wa chakula nyumbani kumewafanya kujitosa kwenye ulingo huo.
Hyline Kwamboka, mmoja wa wajane hawa, amesimulia jinsi ugumu wa maisha na ukosefu wa kazi uliofanya kazi hii kuwa lazima.
"Bwanangu aliaga dunia na kuniacha na watoto saba. Sikuwa na kazi rasmi ya kufanya, na watoto lazima wangesomeshwa, na pia chakula kipatikane nyumbani. Sikuwa na budi ila kuinua nyundo kupasua mawe," anasema Kwamboka.
Wajane hawa wanaanza kazi hii kwa sababu ya ukosefu wa kazi na uwezekano wa kupata riziki, na kazi hii ina madhila yake kabambe, ikiwa ni pamoja na majeraha na uvumilivu wa aina yake.
Wanawake hawa wanaeleza kuwa bei ya mawe yao ni ya chini, ikilinganishwa na kazi nzito waifanyao, na kwa muda mrefu. Wanaeleza kuwa bei inaazia shilingi elfu moja na mia tano hadi elfu tatu, kutegeme na uelewano kati ya mnunuzi na mwuzaji.
Getrude Kerubo, mmoja wa wajane hawa, anasema kuwa sababu kuu ya kumfanya afanye biashara hii ya mawe ni ukosefu wa chakula na ardhi mbaya.
"Huku kwetu chakula hakikiui vizuri. Ardhi hii ni mbaya, hata upande kwa kutumia mbolea nyingi, bado mazao ni mabaya. Hivyo huwezi kutegemea kilimo cha shambani kupata chakula," anasema Kerubo.
Watoto pia wamejaa miongoni mwa wajane hawa, wakiwa katika shule za msingi na wachache katika shule za upili. Wamejaa miongoni mwa kina mama hawa, na wanaeleza kuwa kazi hii ina madhila yake kabambe, ikiwa ni pamoja na majeraha na uvumilivu wa aina yake.