Skip to main content

Mkewe Papa Shirandula, ashtumu Karen Hospital kwa utepetevu wao.

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

This archive report was first published on 20 July 2020.

Mkewe Papa Shirandula, ashtumu Karen Hospital kwa utepetevu wao.

Wakati wa karamu ya mazishi ya Papa Shirandula katika Busia siku ya Jumatatu, Julai 20, 2020, mjane huyo akiwa mwingi wa uchungu alisema marehemu alikata roho katika sehemu ya kuegesha magari ya hospitali hiyo na hakuwa amelazwa.

Alisema nguli huyo alipimwa ugonjwa wa COVID-19 pekee wakati alikimbizwa hospitalini, huku aliongeza kuwa madaktari walipuuza kumfanyia vipimo vingine viwili muhimu (malaria na numonia) ambavyo vingesaidia katika kuokoa maisha ya mume wake.

Alisema, "COVID-19 yaweza kudhibitiwa. Papa alitakiwa kufanyiwa vipimo tatu, virusi vya corona, numonia na malaria. Wakati niliwauliza madaktari endapo walifanya vipimo hivyo, walisema hapana. Niliwauliza mbona walizingatia COVID-19 pekee na huenda alikuwa akiugua ugonjwa mwingine," alisema mjane huyo.

Shemeji yake Rowland Wanyama alisema muigizaji huyo alianza kuugua baada ya kutoka kwa ziara yake katika Kaunti ya Kakamega, na aligunduliwa kuwa na COVID-19 na kukubaliana na madaktari kuwa atarejea nyumbani na kujitenga.

Wiki moja baadaye Papa alikumbana na matatizo ya kupumua na alikimbizwa katika Hospitali ya Karen Hospital na mke wake Ebbie.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →