Skip to main content

Mbunge Junet Mohammed kwenye hatari ya kukamatwa na EACC kuhusu NYS

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

This archive report was first published on 20 July 2020.

Mbunge Junet Mohammed kwenye hatari ya kukamatwa na EACC kuhusu NYS

Julai 20, 2020 - Mbunge wa Suna Mashariki, Junet Mohammed, anachungulia hatari ya kukamatwa na maafisa wa Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi (EACC) kuhusiana na sakata ya Shirika la Huduma za Vijana kwa Taifa (NYS).

Junet, ambaye ni mshirika mkuu wa kiongozi wa ODM, Raila Odinga, anasemekana alinufaika na fedha zilizofujwa kama ilivyoripoti gazeti la Taifa leo Jumatatu.

Junet alihusishwa na kampuni mbili mnamo 2015, ambazo zilisambaza bidhaa za KSh129 milioni kupitia zabuni za NYS ambazo ziliibuwa utata.

Maafisa wa EACC wanachunguza kwa makini zabuni ambayo ilipeanwa kwa kampuni ya Zeigham Enterprises ambapo Junet ni mmoja wa wakurugenzi wakuu pamoja na kaka yake Hussein Mohamed Haji.

Uchunguzi wa EACC unadai kiasi ya pesa za zabuni hiyo zilitumwa katika akaunti ya benki ya Waziri Msaidizi wa Michezo Hassan Noor Hassan, na ya mke wake Meymuna Sheikh Nuh ambaye ni dada yake Junet.

Uporaji wa KSh1.9 bilioni ulikuwa wakati wa muhula wa kwanza wa Rais Uhuru Kenyatta Uongozini.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →