Skip to main content

Dada yake Steve Mbogo na mumewe washtakiwa kulaghai kampuni KSh18.5M

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

This archive report was first published on 19 July 2020.

Dada yake Steve Mbogo na mumewe washtakiwa kulaghai kampuni KSh18.5M

Julai 17, 2020 - Jennifer Mbogo, dada yake mwanasiasa Steve Mbogo, pamoja na mume wake Nathan Loyd Ndung'u, walifikishwa mahakamani kwa ulaghai wa KSh18.5 milioni.

Washtakiwa hao wanadaiwa kushirikiana kuilaghai Kampuni ya Ezetel Kenya kwa kujifanya kama wakurugenzi wa Kampuni ya Avo-veg Health Kenya na kuonyesha uwezo wa kushirikiana na kampuni hiyo kuuza matunda ya parachichichi nje ya nchi.

Washtakiwa hao pia wanashtumiwa kwa kutoa hundi 13 za KSh990,000 mnamo Machi 28 ambazo zilikatatiliwa na benki.

Wakili wa washtakiwa, Mercy Kinyua, alieleza kuwa walimlipa mlalamishi KSh1.6 milioni na tayari wametoa hundi la KSh5 milioni ambalo litatolewa kwa kampuni hiyo mnamo Agosti 31, huku wakitafuta dhamana isiyokuwa na masharti makali.

Walishikilia kuwa hawana njama yoyote ya kuilagahi kampuni hiyo na wana biashara nyingi jijini ambazo zinawafunga kuingia mitini endapo wataachiliwa huru.

Lakini wakili anayewakilisha kampuni ya Ezetel Kenya alikanusha madai kuwa mteja wake alipokea malipo ambayo washtakiwa wanadai.

Katika uamuzi wake, Hakimu Bernard Ochoi alisema wawili hao watasalia kwenye seli ya polisi hadi atakapotoa uamuzi kuhusu dhamana yao siku ya Jumatatu.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →