This archive report was first published on 18 July 2020.
Ikulu yatuma rambirambi kwa familia ya Bukeko ¶
Rais Uhuru Kenyatta alituma rambirambi zake kwa familia ya Charles Bukeko baada ya kufariki dunia.
Ujumbe kutoka Ikulu ulisema Rais aliungana na Wakenya wangine kutuma pole zao kutokana na kuangamizwa kwa muigizaji huyo na ugonjwa wa coronavirus.
Naibu Rais William Ruto alisema kifo hicho ni pigo kubwa kwani Bukeko alikuwa na kipawa cha kipekee.
"Tunahuzunishwa na kifo cha muigizaji machachari Charles Bukeko ‘Papa Shirandula’," Ruto alisema.
"Uigizaji wake utabakia kusisimua na kuhamasisha vizazi vijavyo," aliongeza DP kuhusu maisha ya Papa Shirandula.
DP Ruto aliongeza, "Tutabaki kukosa kazi yake kwenye runinga na kwingineko. Tunaiombea familia yake, marafiki na nyanja ya uigizaji,".
Kinara wa Wiper Kalonzo Musyoka vile vile alimuomboleza msanii huyo kama mtu aliyekuwa na uigizaji wenye mvuto.
Gavana wa Mombasa Hassan Joho alisema kaunti yake ilikuwa imehuzunika baada ya kupata ripoti za kifo hicho.
Ikulu ilituma rambirambi kwa familia ya Bukeko baada ya kufariki dunia.