This archive report was first published on 17 July 2020.
Rais Uhuru Kenyatta alipata mchango wa furaha kutoka kwa msichana wa miaka 20 aliyemchangamkia kupata kazi kupitia mradi wa Kazi Mtaani.
Msichana huyo, Shiro, alipata fursa ya kuzungumza na Rais Uhuru kupitia simu baada ya kuchangamsha Rais kwa maneno na furaha yake ya kupata kazi kupitia mradi huo.
Alimuomba Rais wakutane moja kwa moja huku Uhuru akiahidi kupanga na kutembea Elburgon.
Uzinduzi wa mradi wa Kazi Mtaani ulifanyika Elburgon, kaunti ya Nakuru, na katibu katika Wizara ya Barabara, ujenzi na miundo misingi nchini Charles Hinga.
Msichana Shiro alipata fursa ya kuzungumza na Rais Uhuru baada ya kuchangamsha Rais kwa maneno na furaha yake ya kupata kazi kupitia mradi wa Kazi Mtaani.
"Naongea na Rais?" Wanjiru aliuliza Rais huku akiwa amechangamka kiasi kikubwa.
"Habari ya Elburgon?" Rais alisema huku Wanjiru akizidi kumpa heko kwa kuwapa kazi.
Msichana Shiro alimuomba Rais waonane huku Rais Uhuru akisema vijana wanaofaidika na mradi huo watakuwa wakifanya kazi kwa siku 11 ili wengine pia wapate nafasi hiyo.
"Si kukataa, lakini tunataka tufikie vijana wengi iwezekanavyo. Wewe Shiro ufanye 11 na kisha mwingine, tena wewe urudi zingine 11 hivyo hivyo," alisema Rais.
Uhuru aliahidi kupanga kukutana na msichana huyo atakapotembea eneo la Elburgon.
"Haya wacha tutaona, nitakuja kuwatembelea," Uhuru alimwambia msichana huyo baada ya kusema ana.