Skip to main content

Familia yampoteza mtoto wao baada ya kuvamiwa na chui akichunga

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

This archive report was first published on 17 July 2020.

Chui wakali wa porini wamekuwa kikwazo kikubwa kwa wakazi wa Kajiado, na kifo cha mvulana mmoja kati yao kama hicho kinaibua wasiwasi mkubwa.

Julai 17, 2020, asubuhi, familia moja ilipoteza mvulana wao baada ya chui mweusi kushambulia na kumfua wakati wa kuchunga mifugo katika eneo la Orgira, Kajiado.

Joshua Marine, mmoja wa jamaa wa familia, alisema kisa hicho kilifanyika wakati mvulana huyo na wenzake walikuwa wakichunga katika eneo hilo.

Chui mweusi aliyehusika aliingia mitini baada ya mashambulizi huku wakazi wakiteta kuwa si mara ya kwanza kwa kisa kama hicho kutokea.

Wakazi wa Kajiado walisema wamekuwa wakihangaishwa na wanyama pori wakali kama simba na wengine.

Kamanda wa polisi kaunti ndogo ya Mashuru Ahmed Hillo alidhuibitisha kisa hicho.

Mwili wa mwathiriwa ulipelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya rufaa ya Kajiado.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →