This archive report was first published on 17 July 2020.
Upepo mkali ulipuuza familia tatu katika eneo la Mtwapa, Kilifi, baada ya mapaa ya nyumba zao kuharibiwa usiku wa kuamkia Ijumaa, Julai 17, 2020.
Alhamisi, idara ya utabiri wa hali ya hewa ilitoa tahadhari ya kuwepo kwa upepo mkali na mawimbi makali katika kaunti za Marsabit, Turkana, Samburu, Mandera, Wajir, Isiolo, Garissa, Kitui, Makueni, Taita Taveta, Tana River, Lamu, Kilifi, Mombasa, na Kwale.
Bi Tatu Jumwa, aliyeshuhudia tukio hilo, alisema walisikia kelele mwendo wa saa moja usiku kutoka kwa majirani wao.
“Nyumba moja kati ya zilizoharibiwa ni jirani na yangu. Iko mara mbili; sehemu ya mbele inakaliwa na baba na vijana wawili na sehemu ya nyuma iko na familia ya watoto saba na wazazi wao,” akasema Bi Jumwa.
Wahasiriwa wameomba msaada kutoka kwa wenye uwezo walio na moyo wa kusaidia.
“Tunaomba msaada kutoka kwa wenye moyo wa kusaidia kuturekebishia paa hili. Jinsi muonavyo paa lililokuwa ni hafifu na sasa tunataka paa madhubuti ambalo litavumilia upepo mkali ambao unaendelea kushuhudiwa,” akasema Bw Henry Chengo.