This archive report was first published on 17 July 2020.
Maabara ya Lancet Kenya Kuchunguzwa ¶
Waziri wa Afya Mutahi Kagwe ameagiza uchunguzi kuanzishwa dhidi ya maabara ya Lancet Kenya kwa kutoa matokeo tatanishi ya Covid-19.
Alisema hili Julai 17, 2020, wakati wa kikao na wanahabari kaunti ya Nakuru siku chache baada ya shule ya St Adrew's Turi kuteta kuhusu matokeo ya wafanyakazi wake.
Maabara ya Lancet jijini Nairobi inadaiwa kutoa matokeo ya Covid-19 yanayokinzana na yale ya KEMRI.
Waziri Kagwe alisema maabara ya Lancet Kenya itachunguzwa kwa sababu ya matokeo yake tatanishi.
Alisema, "Ni kweli kuna maabara moja ya Lancet ambayo matokeo yake yaligeuka. Na ni maabala hiyo pia ilikuwa na kisa kama hivyo kwa watu fulani Nairobi."
Alisema pia, "Wizara itachukua hatua zake na pia tumeitaka bodi kuchukua hatua. Lakini pia nataka niwaombe msiende kwa maabala kama hiyo. Kwa nini uende maabara inayotoa matokeo tata?"
Maabara ya Lancet Kenya inadaiwa kutoa matokeo ya Covid-19 yanayokinzana na yale ya KEMRI.
Wafanyakazi 18 wa shule ya St Andrew's Turi walipatikana na virusi vya Covid-19 baada ya kukaguliwa katika maabala ya Lancet lakini mambo yakabadilika baada ya sampuli kupelekwa KEMRI.