This archive report was first published on 16 July 2020.
Mwanamuziki Maarufu Slen Akipigwa na Nguvu za Umeme Kisii, Anahitaji Damu ya Kundi la A ¶
Alamaarufu Slen, mwanamuziki kutoka Kisii, alikanyaga waya ya stima Juni 22 akiwa njiani na marafiki wake wakielekea kazini, na kufanywa huduma za kwanza katika hospitali ya rufaa ya Kisii kabla ya kusafirishwa hadi hospitali ya Kenyatta.
Mkewe wa Slen alisema na TUKO.co.ke kuwa alikimbizwa katika hospitali ya Kisii ambapo alifanyiwa huduma za kwanza kabla ya kusafirishwa hadi hospitali ya Kenyatta.
Mkewe wa Slen alisema, "Alikuwa na marafiki wake wakielekea kazini, akiwa njiani aliganyaga waya ya stima iliyokuwa imewekwa barabarani karibu na eneo la Masota kaunti ya Kisii, alikimbizwa katika hospitali ya rufaa ya Kisii ambapo alifanyiwa huduma ya kwanza kabla ya kusafirishwa hadi KNH."
Kwa sasa, Slen anahitaji damu ya kundi la A, na familia yake imeowaomba wahisani wajitokezea pia katika kuchanga pesa zitakazo gharamia matibabu yake.
Mkewe wa Slen pia alifichua kuwa madaktari katika hospitali hiyo wamekuwa wakimuhudumia vilivyo ingawa alichomeka sana na anaamini atapata nafuu hivi karibuni.
Mkewe wa Slen amewataka wahisani wajitokeze ili wamtolee damu ya kundi la A ambayo anahitaji.
Vile vile, mkewe alisema kuwa bili ya hospitali imepanda sana na angependa wasamaria wema wachange chochote walicho nacho ili aweze kugharamia matibabu yake.
Mkewe wa Slen pia amewashukuru wasanii akiwemo Rose Nyabate na wengine ambao wamesimama nao wakati huu mgumu.
Ili kumsaidia Slen, wasiliana na mkewe kupitia nambari ya simu 0717538467 au unaweza watembelea katika hospitali ya KNH ili kutoka damu.