This archive report was first published on 16 July 2020.
Wizara ya Afya ya Kenya: Wagonjwa 570 Wapona COVID-19 Kwa Siku Moja ¶
Wizara ya Afya ya Kenya ilitangaza kuwa wagonjwa 570 waliopata nafuu kwa siku moja mnamo Alhamisi, Julai 16, 2020.
Waziri wa Afya Mutahi Kagwe alisema wagonjwa 512 kati yao walikuwa wakihudumiwa nyumbani kwao huku wengine 58 wakipokea matibabu hospitalini.
Waziri Kagwe alitoa wito kwa wale wanaotaka kupimwa COVID-19 kuepukana na maabara yanayotoa matokeo ya kukanganya.
Idadi ya wagonjwa wa maradhi hayo nchini Kenya sasa imefika 11,637.
Waziri wa Afya Mutahi Kagwe alisema serikali inafanya uchunguzi ili kuepukana na visa vingine kama hivyo siku za usoni.
Alisema wizara itachukua hatua kuhusu maabara ya Lancet ambayo imekuwa na visa vingi vya kutoa matokeo ya vipimo vya kutatanisha.